Dunia ina satelaiti nyingi zilizotengenezwa na binadamu zinazoizunguka, ingawa ina satelaiti moja tu ya asili inayoizunguka ambayo ni Mwezi. Galaxi yetu ya Njia Maziwa – pia ina satelaiti zake za asili zinazoizunguka. Satelaiti hizi huitwa galaxi mbilikimo “dwarf galaxies” kwa sababu ni ndogo zaidi ukilinganisha na galaxi yetu na cha kufurahisha zaidi ni kwamba wanaastronomia wameipa jina la Wingu Kubwa la Magellanic moja kati ya galaxi mbilikimo zinazoizunguka galaxi yetu.
Wingu kubwa la Magellanic lina eneo kubwa ambamo nyota nyingi huzaliwa. Moja kati ya nyota hizo imeonyeshwa katika picha. Picha iliyochukuliwa na Telescope ijulikanayo kama Telescopve Kubwa Sana, ambayo ipo nchini Chile katika bara la Amerika ya Kusini.
Kiwanda cha kutengeneza nyota kinapatikana ndani ya pete nyekundu. (bonyeza picha ili kuona pete yote). Pete hii ni wingu la gesi na vumbi, liitwalo povu kubwa. Povu hili kubwa lina umbo la pete kutokana na dhoruba zilizowahi kuikumba. Upepo wa kimbunga kutoka katika nyota kubwa na milipuko ya nyota zinazokufa zimesababisha sehemu ya kati kati kuwa tupu na kuacha sehemu ya nje ionekanayo kama pete.
Hata hivyo kutokana na dhoruba zilizoikumba nyota mpya zimeweza kuzaliwa. Upepo na milipuko imesababisha gesi na vumbi kukaribiana katika kingo za povu kubwa. Na pale ambapo gesi na mavumbi ya kutosha yamekutana katika eneo moja basi nyota mpya ilizaliwa. Kwani nyota ni mkusanyiko mkubwa wa gesi na vumbi za angani! wakati nyota zingine zinakufa, nyota nyingine zinazaliwa ambao ni mzunguko wa maisha huko ulimwenguni.
Dokezo
Upana wa povu hili kubwa ni zaidi ya mara 60 ya umbali kutoka kwenye Jua kuelekea kwenye yota ya jirani kabisa!
Share: