Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
SEHEMU ZILIZOJIFICHA ZA MAKAZI YETU MAPYA MWEZINI.
2 November 2017, Dar-es-salaam

Mtazamo wa watu wengi juu ya maisha yetu ya baade huko angani ni vyombo vinavyoelea angani, mahema katika uso wa Mwezi na majengo yenye umbo la Uyoga. Lakini kama una ndoto za maisha mapya nje ya Dunia yetu, basi unaweza kutaka kubadili mtazamo wako. Mapango ya chini kwenye uso wa mwezi yanaweza kuwa makazi ya kifahari kwa wakati ujao!

Mwezi ni jirani yetu wa karibu. Inachukua siku tatu tu kusafiri kutoka Duniani hadi mwezini, ni wazi kuwa hii ni sehemu lengwa kwa makazi mapya ya kutokea nyumbani (Duniani).

Kusaidia kuifanya ndoto hii kuwa kweli, wanasayansi wamekuwa wakifanya utafiti kwenye mahandaki yanayoweza kupatikana katika Mwezi.

Picha za uso wa Mwezi zinaonyesha msururu wa matundu yaliyotoboka, yanayo ashiria uwepo wa mapango na mahandaki yaliyojificha chini yake. Mahandaki haya yanaweza kuwa ni sehemu  ya mitandao mikubwa yenye uwezo wa kutosha  kujenga mitaa na hata miji kwa ajili ya watafiti wa siku zijazo.

Licha ya kuwa Mwezi upo jirani na sisi, mazingira yake ni hatarishi kwa maisha ya Binadamu ukilinganisha na Duniani. Jotoridi katika uso wa Mwezi huweza kushuka chini mara mbili ya jotoridi la ncha ya Kusini ya Dunia au kuwa juu mpaka 100°C! Hii ni kwa sababu mwezi hauna angahewa kama tulilokuwa nalo hapa Duniani.

Kuishi mapangoni chini ya uso wa mwezi kunaweza kutulinda dhidi ya jotoridi hatarishi, kutukinga dhidi ya magimba/miamba inayodondoka kutoka angani na kuzuia miale hatarishi ya Jua. Pia, mapango haya yanaweza kuwa yanafaa kwa maisha ya viumbe kutoka nje ya Dunia ambao wanaweza kuwa wanaishi katika Mwezi au Sayari ya Mars.

Kufahamu zaidi kuhusu mapango ya chini ya ardhi kwenye Mwezi, wanasayansi wanachunguza mapango yanayofanana nayo hapa Duniani. Kama ilivyo kwa mapango ya Mwezini, haya ya hapa yalitengenezwa miaka mingi iliyopita, kutokana na uji wa volkano uliosambaa chini ya ardhi.

Wanaastronomia wanapewa mafunzo katika mapango ya hapa Duniani, wanajifunza namna ya kufanya tafiti ambazo watahitaji kuzifanya wakati wa mikakati ijayo ya kuchunguza Mwezi au Mars.

Dokezo

Ili kuyaona mapango yaliyopo kwenye uso wa mwezi, tutahitaji kimondo kuligonga au kulitoboa paa la pango, ili kudhihirisha mahandaki yaliyofichika chini yake. 

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

Lava Tubes in Lanzarote
Lava Tubes in Lanzarote

Printer-friendly

PDF File
1.0 MB