Find Us Online At
iBookstore
Android app on Google Play
Like Us
A programme by
MKIA WA KIMONDO KINACHOPOTEA
31 August 2017, Dar-es-salaam

Mara nyingi, katika mwaka, anga la usiku humulikwa kwa mamia ya vimondo vinavyowaka. Unaweza kuvifahamu hivi kama “nyota zinazotembea”, ingawa havina uhusiano wowote na nyota. Kwani ni vipande vidogo vidogo vya miamba viunguavyo katika angahewa , ambavyo tunaviita “Vimondo”.

Kuna wakati, Vimondo humurika Dunia katika makundi makubwa kama matone ya mvua. Hii huitwa “Mvua ya Vimondo”

Mvua za vimondo husababishwa na vimondo vidogo vidogo (comets). Vimondo vimetengenezwa na vumbi la angani, miamba na barafu. Vinaposafiri karibu na Jua joto la Jua hupelekea barafu kuyeyuka. Hivyo vipande vidogo vya miamba na vumbi huchomoka na kutengeneza mikia mizuri yenye kuwaka.

Wakati Dunia ikiwa inasafiri kukatiza mikia ya vimondo hivi, vipande vyake  huungua katika angahewa la Dunia na kutengeneza mvua ya Vimondo.

Moja kati ya mvua za kupendeza za vimondo ni “Phoenicids” (inatamkwa “FEE-ni-kids”). Phoenicids iliangaza anga letu mwaka 1956…..na haijawahi kujirudia tena. Wanaastronomia waliachwa na bumbuwazi: ni wapi mvua ya Phoenicids ilitokea na ni wapi ilitokomea?

Katika kutafuta jibu la swali hili, walienda kutafuta kimondo kilichopotea kiitwacho Blanpain.

Mwaka 1819, wanaastronomia wawili walikigundua Kimondo Blanpain. Lakini mwisho wa mwaka kilipotea kimaajabu.

Baada ya miaka takribani 200 kupita, kimondo kikubwa kilionekana kikisafiri katika njia sawa na ile ya kimondo Blanpain.

Mabarafu, gesi na mavumbi yote ambayo huenda yaliponyoka kutoka kwenye kimondo, bado yanaelea ulimwenguni kama mchirizi mwembamba wa vumbi unaoelea. Pia kama kimondo kikubwa yanafuata njia ileile iliyopitiwa na kimondo cha Blanpain.

Pindi mchirizi huu wa vumbi la kimondo Blanpain unapogongana na Dunia, vipande vyake huliangaza anga kama mvua ya vimondo (Phoenicid)!

Dokezo

Vitu vinavyotengeneza mvua ya vimondo angani, vyote hutoka katika uelekeo mmoja. Mvua za vimondo nyingi hupewa majina kutokana na makundi-nyota ambayo huwa zinatokea. Lakini, kwa uhalisia zilizopo katika kundi-nyota zipo mbali zaidi kuliko zionekanavyo.

Share:

More news
12 October 2020
1 October 2020
16 September 2020
14 September 2020
10 September 2020

Images

Geminid Meteor Shower
Geminid Meteor Shower

Printer-friendly

PDF File
1.2 MB