Mwaka 2009, mwanamke mmoja nchini Marekani alivunja rekodi ya Dunia ya kujifungua watoto wengi katika uzao mmoja, alipojifungua watoto nane wenye afya njema kwa pamoja.
Katika kundi la wanyama, rekodi inashikiliwa na farasi-bahari dume ambaye anaweza kubeba vitoto hadi 2,000 kwa wakati mmoja kabla ya kuvizaa. Hata hivyo, mshindi wa kweli wa tuzo ya “Mama wa mwaka” ni nebulae.
Nebula ni mawingu ya gesi na mavumbi yaliyopo angani, ambamo mabilioni ya nyota mpya huzaliwa. Kama ilivyo kwa Farasi-bahari, nyota huzaliwa katika idadi ya maelfu, kutoka katika kundi moja la wingu moja kwa wakati mmoja.
Picha hii ya ulimwengu inaonesha wingu maarufu ambamo nyota huzaliwa angani linaloitwa, “Orion Nebula”. Unaweza kuona michirizi ya mawingu ya gesi yenye rangi rangi, yanayotengeneza hiyo pamoja na maelfu ya nyota mpya zilizozaliwa.
Nebulae ya Orion imekuwa kivutio cha binadamu kwa maelfu ya miaka, lakini bado tunaendelea kuvumbua siri zake mpya hadi leo. Kwa kutumia picha hii iliyopigwa angani kupima ung’avu na rangi za nyota, wanasayansi waliweza kukokotoa umri usahihi wa nyota zake.
Imegundulika kuwa licha ya nyota hizi zote kuwa zimezaliwa katika wingu moja (Nebula ya Orion), zimegawanyika katika makundi matatu ya umri. Kila kundi lilitengenezwa kwa wakati wake tofauti. Hivyo,licha ya nyota hizi kuwa ni ndugu wa “Mama” nebula mmoja, zina umri tofauti tofauti!
Dokezo
Pia imegundulika kuwa kila kundi kati ya haya matatu ya vizazi tofauti linazunguka kwa mwendokasi tofauti– nyota changa zina nishati nyingi zaidi hivyo huzunguka kwa kasi zaidi, wakati nyota kongwe hujizuka katika spidi ndogo.
Share: