Kama umewahi kuwa na kitu kizuri katika maisha yako, huwa ni kitu cha kawaida kutojua thamani yake…hasa kama kitu hicho hakionekani kwa macho. Lakini leo inatupasa kuchukua muda na kutafakari ni bahati gani tuliyonayo kwa sayari yetu kuwa na tabaka la hewa!
Tabaka la hewa la Dunia limetengenezwa na gesi zinazoizunguka Dunia kama blanketi, na zimeshikiliwa na nguvu ya uvutano ya gravity. Hufanya jotoridi la Dunia kuwa zuri: huzuia baridi kali la angani wakati wa usiku na joto kali la Jua wakati wa mchana. Zaidi ya hapo tabaka la hewa linafanya kazi kama ngao, kwa kufyonza miale hatari inayotoka kwenye Jua na vitu vingine vya angani kabla haijafika katika uso wa Dunia!
Imejulikana kuwa baadhi ya sayari zilizo nje ya mfumo wetu wa Jua nazo zina matabaka ya hewa! Wanaastronomia nchini Japani wamegundua tabaka la hewa la sayari inayozunguka nyota nyingine iliyopo mbali. Sayari hii ni kubwa wa mara 4 ukilinganisha na Dunia. Tunaziita sayari kama hizi Dunia Kubwa “Super-Earths”. Uchunguzi umeonyesha kuwa wakati sayari hii inadhaniwa kuwa na tabaka kubwa la hewa, ambalo ni zito zaidi ya mara 200,000 kuliko la Dunia, haijazungukwa na mawingu. Nafikiri wengi wenu mtakuwa mnaionea wivu!
Dokezo
Hakuna mpaka halisi kati ya tabaka la hewa na anga, kwa sababu tabaka la hewa huongezeka kuwa jembamba kadri linavyozidi kutanuka. Ingawa tumeweka mstari wa kufikirika katika kilometa 100 kwenda juu, ambapo baada ya hapo anga inaanza. Tunauita mstari huu Kármán. Lakini kama binadamu tunaweza kupumua mpaka katika kilometa kama 8.
Share: