Nyota za Neutron ni viini vizito zinavyobakia baada ya nyota kubwa kufa na kulipuka huko angani. Matabaka ya nje ya nyota hurushwa mbali katika milipuko hiyo, lakini maada katika viini vya nyota hizo husambaratika vyenyewe na hutengeneza burungutu kubwa la maada. Kinachobakia baada ya hapo ni kitu kilichokandamizwa chenye mkandamizo mkubwa katika ulimwengu wote nje shimo jeusi: nyota ya neutron!
Picha hii mpya iliyopigwa huko angani inaonyesha kundi la nyota lijulikanalo kama ‘globular cluster’. Ambayo ni baadhi tu ya vitu ambavyo ni vya kale sana huko angani— umri wake unakaribiana kabisa na umri wa ulimwengu wenyewe! Hii inamaanisha kuwa nyota nyingi zilizopo ndani yake zimeshakufa. Na zile kubwa zaidi zimekwishalipuka na kuacha nyota za neuton.
Kwa kutumia nyota ya neutron katika kundi hili pamoja na nyingine nyingi, wanaastronomia wameweza kutambua uhusiano kati ya uzito wa nyota (kiasi cha maada inayobeba) na ukubwa wake.
Taarifa mpya zinaonyesha kuwa nyota ya neutron ya kawaida, yenye uzito wa mara moja na nusu ya Jua letu inaweza kuwa na kipenyo cha kilometa 12. Urefu ambao ni karibu sawa na eneo la mji mdogo! Likiwa na maada zote hizi zimekandamizwa katika sehemu hiyo ndogo. Hivyo basi nyota za neutron ni nzito mno. Nguvu ya mkandamizo (Presha) katika kiini chake ni zaidi ya trilioni kumi kuliko nguvu ya mkandamizo inayohitajika kutengenezea almasi ndani ya Dunia.
Dokezo
Nyota za neutron zimepakiwa na kukandamizwa sana hivyo kuzifanya ziwe na duara pete. Mlima unaoweza kutokea katika uso wake unaweza kuwa na urefu wa milimita 5 tu!
Share: